Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2022

 M.ADA YA WIKI: Je, miundombinu ya  shule Tanzania inaruhusu elimu jumuhishi? Unaweza  kuchangia mada hii hapohapo kwenye blog au kupitia zawadimsigala1@gmail.com Pia unaweza kuomba ushauri kuhusu watu wenye ulemavu kupitia hiyo hapo juu
                 ZAWADI NA NYUMBA ALI SEHEMU YA 2.      Katika sehemu ya kwanza nilisema kuwa sababu za kuanzish shirika nitazieleza hapo baadaye, sasa naomba niwaeleze sababu za kuanzisha shirika la nyumba Ali. Bi Bruna na Bwana Lucio walifika hapa nchini Tanzania kwa mara ya kwanza mnamo mwaka   2006 kwa lenngo la kupata mapumziko.   Baada ya kufika   hapa nchini walikuta changamoto kubwa ya watoto wenye ulemavu, waliguswa sana na changamoto hizo ndipo walipo rudi nyumbani kwao Italia walianza kuunda shirika la nyumba Ali huku wakiwa na lengo la kuwasaidia   watoto wenye ulemavu nchini, bila shaka changamoto za watoto wenye ulemavu ndizo sababu za kuanzisha shirika hili.    Mimi kama Mtanzania ambaye pia ni mnufaika wa shirika hili nawapongeza na kuwashukuru Bi Bluna na Bwana Lucio kwa kuanzisha shirika hili ambalo limekuwa msaada mkubwa kwetu watu wenye ulemavu nchini. Sehemu ya tatu itaelezea namna gani shirika limenisaidia mimi Zawadi Msigala.                 USIKOSE SEHEM
  ZAWADI NA NYUMBA ALI.         Nyumba Ali ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kulea   watoto wenye ulemavu katika manispaa ya Iringa. Shirika hili lilianzishwa mwaka 2007 na raia wawili wa kitaliano ambao ni bi Bruna na bwana Lucio. Sababu za kuanzisha nitazieleza hapo baadaye.   Huduma zitolewazo na shirika hili ni pamoja na mazoezi ya viungo, huduma za afya kwa watoto wenye ulemavu, wenye shida za kiafya, lishe bora kwa watoto wenye ulemavu, huduma ya makazi   kwa watoto   wenye ulemavu wenye mazingira magumu, huduma ya elimu kwa watoto wenye uwezo wa kusoma na huduma ya kuwapa elimu ya ufundi stadi kwa watoto wasio na uwezo wa   kusoma.    Zawadi Msigala ambaye pia ni mmiliki wa jukwa hili ni kijana ambaye ninajivunia mafanikio makubwa ya kielimu licha kuwa ni mtu mwenye ulemavu. Mafanikio haya nimeyapata kutokana na msaada mkubwa wa shirika la Nyumba Ali, nilianza kuhudumiwa na shirika hili mwaka 2009.                 USIKOSE MUENDELEZO WA SIMULIZI HII.
Jina langu ni Zawadi Msigala, ni mtanzania ninayeishi na ulemavu wa viungo, pia ni mwanaharakati wa haki za walemavu hapa nchini.  Nimeamua kufungua jukwaa hili ili nishirikiane na watanzania wenzangu katika kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali za watu wenye ulemavu. Kwa muda huu sitakuwa na mengi ya kusema, nitaendelea kuwa nanyi kupitia jukwaa hili. Naomba ushirikiano wenu katika kuzitatua changamoto za watu wenye ulemavu.