ZAWADI
NA NYUMBA ALI.
Nyumba Ali ni shirika lisilo la
kiserikali linalojishughulisha na kulea
watoto wenye ulemavu katika manispaa ya Iringa. Shirika hili lilianzishwa
mwaka 2007 na raia wawili wa kitaliano ambao ni bi Bruna na bwana Lucio. Sababu
za kuanzisha nitazieleza hapo baadaye. Huduma
zitolewazo na shirika hili ni pamoja na mazoezi ya viungo, huduma za afya kwa
watoto wenye ulemavu, wenye shida za kiafya, lishe bora kwa watoto wenye
ulemavu, huduma ya makazi kwa
watoto wenye ulemavu wenye mazingira
magumu, huduma ya elimu kwa watoto wenye uwezo wa kusoma na huduma ya kuwapa
elimu ya ufundi stadi kwa watoto wasio na uwezo wa kusoma.
Zawadi Msigala ambaye pia ni mmiliki wa
jukwa hili ni kijana ambaye ninajivunia mafanikio makubwa ya kielimu licha kuwa
ni mtu mwenye ulemavu. Mafanikio haya nimeyapata kutokana na msaada mkubwa wa
shirika la Nyumba Ali, nilianza kuhudumiwa na shirika hili mwaka 2009.
USIKOSE MUENDELEZO WA SIMULIZI HII.
MADA
YA WIKI: Je, watu wenye ulemavu nchini Tanzania wanapewa haki zao ipasavyo?
Unaweza kuchangia mada hii hapohapo kwenye blog au
kupitia zawadimsigala1@gmale.com.
Pia
unaweza kuomba ushauri kuhusu watu wenye ulemavu kupitia hiyo hapo juu
Good job Zawadi!Go on!
JibuFutaThank you Silvia! I shall go on with my job
Futa