ZAWADI
NA NYUMBA ALI SEHEMU YA 2.
Katika sehemu ya kwanza nilisema kuwa
sababu za kuanzish shirika nitazieleza hapo baadaye, sasa naomba niwaeleze
sababu za kuanzisha shirika la nyumba Ali. Bi Bruna na Bwana Lucio walifika
hapa nchini Tanzania kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2006 kwa lenngo la kupata mapumziko. Baada ya kufika hapa nchini walikuta changamoto kubwa ya
watoto wenye ulemavu, waliguswa sana na changamoto hizo ndipo walipo rudi
nyumbani kwao Italia walianza kuunda shirika la nyumba Ali huku wakiwa na lengo
la kuwasaidia watoto wenye ulemavu
nchini, bila shaka changamoto za watoto wenye ulemavu ndizo sababu za kuanzisha
shirika hili.
Mimi kama Mtanzania ambaye pia ni mnufaika
wa shirika hili nawapongeza na kuwashukuru Bi Bluna na Bwana Lucio kwa
kuanzisha shirika hili ambalo limekuwa msaada mkubwa kwetu watu wenye ulemavu
nchini.
Sehemu
ya tatu itaelezea namna gani shirika limenisaidia mimi Zawadi Msigala.
USIKOSE SEHEMU YA TATU YA
SIMULIZI HII.
MADA
YA WIKI: Nini kifanyike kwa vijana wenye
ulemavu ili waishi kama vijana wengine?
Unaweza kuchangia mada hii hapohapo kwenye blog au
kupitia zawadimsigala1@gmail.com
Pia
unaweza kuomba ushauri kuhusu watu wenye ulemavu kupitia hiyo hapo juu
Maoni
Chapisha Maoni